Create New Playlist

Add a cover pic of your own choice

(Optional)

Name

AI Cover Generator

4 credits

Not enough credits (0/4).

Logout

Are you sure you want to Logout?

Close

Raila Mti Mkuu (Hymn of the Great Tree) 2 by VINCENT OKWETSO

SongGPT
Raila Mti Mkuu (Hymn of the Great Tree) 2 by VINCENT OKWETSO  - Afro-Fusion Ballad,Male Vocals music cover art

Raila Mti Mkuu (Hymn of the Great Tree) 2

Afro-Fusion Ballad,Male Vocals

0:003:50
Lyrics
Description
[Verse 1]
Nyuni wamo mashakani, furaha imetoweka,
Wamesalia shimoni, mwanzo wao kuteseka,
Atawaokoa nani, wana wasije dhikika?
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Chorus]
Pumzika kwa amani, kigogo mpenda haki,
Taifa lina huzuni, na nyoyo zilo na dhiki,
Imeyeyuka imani, wapenziwo halaiki,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Verse 2]
Machozi yamefurika, kama bahari ya shamu,
Kilio kinasikika, magharibi na kuzimu,
Wakenya metamauka, na mamuzi ya Rahimu,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Bridge]
Uliwapea mwangaza, gizani walipozama,
Ujasiri lihimiza, kwa waliokata tama,
Sauti ungeipaza, kuishutumu dhuluma,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Chorus]
Pumzika kwa amani, kigogo mpenda haki,
Taifa lina huzuni, na nyoyo zilo na dhiki,
Imeyeyuka imani, wapenziwo halaiki,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Verse 3]
Sauti yako imara, ilileta tumaini,
Ilidumaza uchwara, uliopingwa nchini,
Fika salama ahera, utasalia nyoyoni,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Verse 4]
Mapambano yako mema, vitabu tutaandika,
Ni ishara yenye wema, alokupea Rabuka,
Ni vipi litasimama, kigogo siposikika,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Chorus]
Pumzika kwa amani, kigogo mpenda haki,
Taifa lina huzuni, na nyoyo zilo na dhiki,
Imeyeyuka imani, wapenziwo halaiki,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Verse 5]
Wakenya uliwapenda, wote ukakumbatia,
Mazuri uliyotenda, Wakenya lifurahia,
Kote wingu limetanda, ni mengi wanawazia,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Bridge 2]
Wimbowo utasalia, kwenye nyoyo za Wakenya,
Mahadhi ya kukuzia, nyoyo zetu yatapenya,
Nani atakurithia, asiwe wa kutufinya,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Verse 6]
Nyuni wameinama, vichwa chini kwa huzuni,
Wameshindwa kusimama, na ukweli kubaini,
Mafumbo liyoyasema, wataishi yatamani,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.
[Outro]
Iifariji familia, kwa kuwapa tumaini,
Ilahi ewe Jalia, wazidishie amani,
Pema mhifadhia, alale pema peponi,
Raila Mti Mkuu, Pumzika kwa amani.