Create New Playlist

Add a cover pic of your own choice

(Optional)

Name

AI Cover Generator

4 credits

Not enough credits (0/4).

Logout

Are you sure you want to Logout?

Close

Nani Atamfunga Paka Kengere 2 by ManA

SongGPT
Nani Atamfunga Paka Kengere 2 by ManA - folk,male vocals music cover art

Nani Atamfunga Paka Kengere 2

folk,male vocals

0:003:22
Lyrics
Description
[Intro]
Mwafrika halisi
[Verse 1]
Hapo zamani za kale kulikua na kijiji kimoja cha panya,
Kijiji kile kilikua na panya wengi na waliendelea kuongezeka siku hadi siku!
Ilitukia siku moja panya wakaanza kupotea,
Na wengine wakakutwa porini na sehemu nyingine wakiwa tayari wamekufa,
Wengine walikutwa wakiwa hawana vichwa, au viungo mbali mbali!
[Chorus]
Nani atamfunga paka kengere?
Nauliza nani atamfunga paka kengere?
Tukomeshe mauaji na utekaji,
Nani atamfunga paka kengere?
[Verse 2]
Mateso yalizidi sana,
Panya waliokua na ndugu zao sehemu za mbali walijitahidi kukimbia hali ile ya hatari,
Hata hivyo katika hali isiyokua ya kawaida muuaji wa panya akajitokeza hadharani
Na siku nyingine alivamia mchana kabisa na kuondoka na panya...
[Chorus]
Nani atamfunga paka kengere?
Nauliza nani atamfunga paka kengere?
Tukomeshe mauaji na utekaji,
Nani atamfunga paka kengere?
[Verse 3]
PAKA! Hakika huyu ndie alikua adui mkubwa wa panya!
Jina la paka likawa maarufu sana katika jamii ile ya panya kwa kipindi kile!
Hatimaye hali ya hatari ikatangazwa na mfalme wa panya
Na siku ya mkutano mkuu ikatangazwa panya wote wakusanyike
Kwa ajili ya kujadiliana juu ya nini kifanyike kumdhibiti yule paka!
[Chorus]
Nani atamfunga paka kengere?
Nauliza nani atamfunga paka kengere?
Tukomeshe mauaji na utekaji,
Nani atamfunga paka kengere?
[Bridge]
Kazini wakae nyumbani kwani sasa dawa ya adui yao imepatikana!
Wakati sherehe zikiendelea mzee gwaya yeye machozi yalikua yakimtoka
Alishindwa hata kusimama na alijaribu kunyoosha mkono wake
Ili atoe wazo lake lakini hakuna aliyemsikiliza
Kila mmoja likua bize kufurahia na mkutano ukaishia pale!
[Outro]
Nani atamfunga paka kengere?
Tukomeshe mauaji na utekaji,
Nani atamfunga paka kengere?