Create New Playlist

Add a cover pic of your own choice

(Optional)

Name

AI Cover Generator

4 credits

Not enough credits (0/4).

Logout

Are you sure you want to Logout?

Close

NAMTUMA NJIWA na Malenga Okwetso 2 by Vincent

SongGPT
NAMTUMA NJIWA na Malenga Okwetso 2 by Vincent - Afrobeat,Male Lead With Female Harmonies Vocals music cover art

NAMTUMA NJIWA na Malenga Okwetso 2

Afrobeat,Male Lead With Female Harmonies Vocals

0:003:46
Lyrics
Description
NAMTUMA NJIWA na Malenga Okwetso
Kigodani nakalia, Okwetso kuwanenea,
Kononi nashikilia, barua nilokomea,
Mwenyewe kamwandikia, njiwa kanipelekea.
Njiwa wewe ukifika, waraka umkabidhi.
Mwambie navyowazia, mawazo menilemea,
Nashindwa kuvumilia, lini yatatokomea,
Au lipi tatumia, mawazo kunondokea,
Njiwa wewe ukifika, waraka umkabidhi.
Wanguwangu jipakia, njiwa uweze pepea,
Nakuomba kasikia, waraka sije potea,
Kwake weza mpatia, huku umenyenyekea,
Njiwa wewe ukifika, waraka umkabidhi.
Ukifika kamwambia, mfereji nalindia,
Hakuna ananuia, maji akiharibia,
Vyema nimehifadhia, maji atayaridhia,
Njiwa wewe ukifika, waraka umkabidhi.
Usije puuzilia, hili wewe kumwambia,
Amba asije kawia, bali aweze wahia,
Aje akanitibia, ndwele zilonifikia,
Njiwa wewe ukifika, waraka umkabidhi.
Waraka namalizia,tuli nenda kutulia,
Jibu kilisubiria, njiwa akijirudia,
Rabi kamtangulia, mawi sije kuvamia,
Jawabu ukishapewa, wanguwangu niletee.