Create New Playlist

Add a cover pic of your own choice

(Optional)

Name

AI Cover Generator

4 credits

Not enough credits (0/4).

Logout

Are you sure you want to Logout?

Close

BURIANI ASKOFU SULUMETI 1 by VINCENT OKWETSO

SongGPT
BURIANI ASKOFU SULUMETI 1 by VINCENT OKWETSO  - Kiswahili Funeral Hymn / Liturgical Choir With Gtr music cover art

BURIANI ASKOFU SULUMETI 1

Kiswahili Funeral Hymn / Liturgical Choir With Gtr

0:003:40
Lyrics
Description
BURIANI ASKOFU SULUMETI
Mwangawe uliangaza, katika taifa letu,
Na wema liueneza , uliowafaa watu,
Wema akautangaza, kijue kizazi chetu,
Likuwa mfano mwema, kwa kondoo alowachunga.
Mpya lijenga imani, ndani ya yetu jamii,
Kaimarisha jimboni, kwa nia yenye bidii,
Huduma alipeani, waumini wakatii,
Alacha matumaini, yaliyotukuka sana.
Shule nyingi alijenga, na kuwalea vijana,
Elimu ikawa mwanga, kufaidi wengi wana,
Hospitali akajenga, kumtibia Rabana,
Makasisi tenda mema, ikafaidi jamii.
Mwanga likuwa thabiti, katika totoro giza,
Alikuwa madhubuti, Dayosisi kuongoza,
Sauti yake ya dhati, hakuwa ya kulemaza,
Hekimaye ilijenga, misingi yenye amani.
Pakubwa alichangia, kwa mijadala mipevu,
Na mengi kaangazia, kwa wingi wa ushupavu,
Kanisa likumbushia, ukweli ulo angavu,
Lisisitiza umoja, kama dira ilo bora.
Aliitetea katiba, ile mpya kwa busara,
Yasofa akarilaba, akanena yalo bora,
Ikakuwa ndio tiba, kulipa taifa fora,
Mola mhifadhi pema, Askofu Sulumeti.
Limtaja viongozi, kuwa mhudumu mwema,
Likuwa mja aazi, mwenye wingi wenye wema,
Hakula kwa ajizi, mali iso ya tama,
Alipanda mbegu njema, kwenye vizazi vya sasa.
Safariye ya huduma, karibia hamsini,
Ilija jasho la wema, ahadi za tumaini,
Likuwa kingozi mwema, alemuenzi Manani,
Na Mola amemuita, buriani Askofu.
Urithi wake wabaki, kuiongoza dunia,
Uzidi kutamalaki, waja kuwahudumia,
Wengi umewaafiki, kwa huduma lowapatia,
Yeye ni shara njema , ya imani nayo wema.
Tuenzi maisha yake, kwa matendo yalo mema,
Tukafuate nyayo zake, za upendo nao wema,
Tushukru Mola wake, kwa hatua ilo njema,
Alale pahali pema, Askofu Sulumeti.